Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama, Jumanne Sagini akikabidhi vyeti na zawadi kwa baadhi ya Walimu waliofaulisha wanafunzi wa shule za Sekondari Butiama.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Walimu wa Butiama walioshiriki kwenye Kikao cha Kufanya Tathmini ya Maendeleo ya Elimu ya Sekondari katika wilaya ya Butiama kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Chief Ihunyo iliyopo Kata ya Busegwa tarehe 10/09/2022
…………………………………..
Na Mwandishi wetu,BUTIAMA
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama, Jumanne Sagini amewaondoa wasiwasi walimu wa Wilaya ya Butiama waliokuwa na hofu ya kiutendaji kufuatia na mauaji ya Mwalimu mwenzao Saidi Saidi Hamisi aliyeuawa mwishoni mwa mwezi wa nane aliyekuwa akifundisha Shule ya Sekondari Masaba iliyopo wilayani humo mkoani Mara.
Akizungumza na walimu walioshiriki katika Kikao cha Kufanya Tathmini ya Maendeleo ya Elimu ya Sekondari katika wilaya ya Butiama, Naibu Waziri Sagini amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshalifanyia kazi na kwamba tayari wahalifu watatu wameshakamatwa na wako ndani wanahojiwa.
Aidha amesema mauaji ya Mwalimu Saidi Saidi Hamisi hayatafasiri kuwa wananchi wa Butiama wanachuki na Walimu bali waliotenda uhalifu huo ni wahalifu wabaya waliomvamia kwa lengo la kupata masilahi binafsi kutokana na kwamba mwalimu huyo alikuwa mfanyabiashara.
“Nawapa pole sana kwa niaba ya Serikali na naomba nisema huu ni uhalifu mbaya lakini isifikie hatua kwamba kundi lote la walimu likasema kwamb mbona tunauawa” alisema.
Naibu Waziri Sagini aliyasema hayo jana aliposhiriki kwenye Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Chief Ihunyo iliyopo Busegwe, Wilayani Butiama.
Pamoja na hayo Naibu Waziri Sagini amewataka walimu wa wilaya ya Butiama kuongeza bidii ya kufundisha na kuzidi kuwapa wanafunzi mitihani kuendana na mitaala na ufaulu wa shule zingine. Amewataka kuacha kuamisha maumivu yao kwa wale waliokuwa chini yao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇