LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 6, 2022

MKUMBUKE HAYATI KAPTENI JOHN KOMBA KUPITIA KITABU CHAKE HIKI

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Wikendi moja marafiki walikutana wakanunua mbuzi wakamchinja kisha wakapikiwa supu mahala hapo walipokutana. Supu ilipokuwa tayari wakaanza kula huku wanapiga soga za hapa na pale.

Ghafla mmoja kati yao akawaambia wenzake, "najisikia kwenda haja, endeleeni kula lakini mnibakishie naenda msalani, nitakuja kuendelea kula". Baada ya kuondoka wenzake wakaendelea kula supu hata wakawa wametosheka, wakambakizia sehemu yake kama alivyowaomba.

Baada ya wao kutosheka wakamsubiri wee! wakatahamaki nusu saa nzima imepita, wakaamua kwenda kumuangaalia huko mslani, Lahaula! walipofungua mlango wa msalani kwa kuuvunja wakakuta mwenzao alishafariki muda mrefu, ni nzi tu ndiyo wame-'mpamba' mwili wote! Wakashikwa na butwaa na kuangua kilio. Naam, amekwisha lala usingizi wa milele!".  

Basi hivyo ndivyo maisha yalivyo, kama tulivyokuja duniani bila kujua, ndivyo pia hatujui muda wala siku ya kuondoka duniani kwenda kwa Mungu Baba, Muumba wa yote na vyote.

Bila shaka waliokaribu na masuala ya Siasa na Burudani, hasa ya nyimbo za kwaya, hivi sasa ninapowatajia jina la aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mbunge na Mkurugenzi wa Kikundi cha Tanzania One Thetre (TOT) Hayati Kapteni John Komba lazima mwili utawasisimka.

Mwili utawasisimka kwa sababu nyingi, lakini kubwa ni namna alivyokuwa karibu na watu wa rika zote na wa kila aina kwa hali na mali na kwa jinsi kiumbe huyu alivyokuwa mahiri katika uimbaji na katika siasa.

Kapteni Komba, alifanya kazi zake kwa juhudi na maarifa na kwa weledi mkubwa, na bila shaka aliweza kuwa ngazi ya kuwafanya wengi kuinuka kisiasa kupitia nyimbo alizokuwa anaimba na pia kuwanua hata baadhi ya watu kimaisha.

Lakini tazama, japo sote tunajua kwamba kifo kipo, hakuna aliyeweza kujua kwamba Kapteni Komba angeiaga dunia muda gani na lini na kurejea kwa Mungu Baba na sasa ni miaka minane na miezi kadhaa tangu Kapteni Komba alipoiaga Dunia Feabruari 28, 2015.

Hivi majuzi nilitembelea nyumbani kwa familia ya Hayati Kapteni Komba, eneo la Mbezi Beach Kwa Komba, Kawe Jijini Dar es Salaam, nikapata kuzungumza kidogo na Mjane Salome John Komba. Yapo mengi tulizungumza lakini ninachoweza kuripoti kwa sasa kwako ni Kitabu cha historia ya Maisha ya Hayati Kapeni Komba ambacho familia ilinionyesha.

 "Mwanangu unakiona kitabu hiki, kina historia yote ya rafiki yako Kapteni Komba", akasema Bi Salome John Komba, huku akinikabidhi Kitabu hicho chenye kujinadi kwa maandishi "MAISHA YA MZALENDO JOHN DAMIANO KOMBA".


Baada ya kukipokea nikakisoma ukurasa kwa ukurasa nikakubaliana na Bi Salome, Mjane wa Kapteni Komba, kwamba kweli kitabu hicho kimesheheni historia ya kutosha ya hayati John Komba, maana kinaeleza tangu kuzaliwa kwake hadi maziko yake.
Kitabu chenyewe hicho👇

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages