Na Mwandishi Maalum, Mwanza
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amehitimisha ziara yake mkoani Mwanza kwa kuzunguzumza na wanachama wa Chama wa CCM katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa.
Mkutano huo ulihudhiriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ambaye amekuwa na Kinana kwenye mikoa yote aliyofanya ziara.
Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Dialo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula, Wabunge, Wajumbe wa NEC, Mku wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima na wanachama wengine wa CCM.
Akizungumza na Wana CCM hao Kinana amewahimiza kuendelea kudumisha umoja na mshikamano huku akikumbusha kuwa kwa sasa Chama kipo kwenye mchakato wa kuchagua viongozi hivyo ni vema wakachagua viongozi wenye sifa za uongozi badala ya kuchagua kwa kuangalia urafiki, ukabila au ukanda.
Katika ziara hiyo Kinana ametembelea mikoa ya Kigoma, Kagera, Geita na Mwanza ambapo pamoja na mambo mengine amekutana amekagua miradi ya maendeleo ukiwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.
Your Ad Spot
Sep 6, 2022
Home
featured
siasa
KINANA AUNGURUMA MWANZA, AHIMIZA WANA CCM KUCHAGUA VIONGOZI WENYE SIFA, SIYO URAFIKI, UKABILA WALA UKANDA
KINANA AUNGURUMA MWANZA, AHIMIZA WANA CCM KUCHAGUA VIONGOZI WENYE SIFA, SIYO URAFIKI, UKABILA WALA UKANDA
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇