LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 6, 2022

MARTHA GWAU ALIA NA WAMACHINGA WALIOPATA AJALI YA MOTO


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Martha Gwau ametoa salamu za pole kufuatia tukio la ajali ya  moto kwenye vibanda vya wafanyabiashara wadogo (Machinga) vilivyopo karibu na Ofisi za Posta Singida Mjini, tukio hilo lilitokea usiku wa Sept 3, 2022 ambapo zaidi ya vibanda 50 vimeteketea.


Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Martha Gwau amesema amesikitishwa na tukio ilo linalokwenda kuathiri maisha ya wajasiriamali hawa kwa namna moja na ukizingatia hakuna kilichookolewa ili ni pigo kubwa 


Naishukuru sana Serikali kuanzia ngazi ya Mkoa mpaka ngazi ya Wilaya kwa namna ambavyo wameendelea kuwa bega kwa bega na wajasiriamali hawa tangia jana ulipotekea moto huu. 


Martha Gwau amewakumbusha pia wananchi kuchukua tahadhari na kutoa taarifa mapema pindi wanapoona matukio haya ya moto yanatokea ili kuweza kudhibiti mapema kabla ya kuleta madhara makubwa


 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages