Na Chiristopher Lissa wa Gazeti la Uhuru
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Wilaya ya Temeke wamemchagua Lawama Mohammmed Mikidadi kuwa Mwenyekiti mpya wa umoja huo wilayani humo.
Katika uchaguzi huo uliofanyika Dar es Salaam, nafasi hiyo ilikuwa na wagombea watatu ambao ni Lawama, Hanifa Kitwana Kondo na Rukia Kamal.
Msimamizi wa Uchaguzi huo ambaye ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, James Mgego amemtangaza Lawama kuwa mshindi kwa kupata kura 333.
"Mgego amesema nafasi ya pili imechukuliwa na Anifa Kitwana Kondo aliyepata kura 143, huku Rukia Kamal akipata kura sita, hivyo ninamtangaza Lawama Mohammed Mikidadi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT Wilaya ya Temeke” akasema Mgego.
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Lawama amewashukuru wajumbe kwa kumuamini kushika wadhifa huo na kwamba yuko tayari kuutumikia umoja huo na Chama Cha Mapinduzi CCM na kuwaomba wajumbe na wanachama wa UWT na Chama kumpa ushirikiano.
Mbunge wa Viti Maalumu Mariam Kisangi, aliwashukuru wajumbe kwa kufanya uchaguzi huo kwa amani.
Mbali na nafasi hiyo ya Mwenyekiti pia UWT wilayani humo ilipata viongozi wapya katika nafasi ya Mjumbe wa MkutanoMmkuu wa Mkoa, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT na wawakilishi wa Mkutano wa Baraza la UWT Mkoa.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya TemekeLawama Mohamed, akizungumza katika Mkutano Mkuu wa umoja huo, baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi uliofanyika katika Ukumbi wa Sabasaba, Dar es Salaam. Kushoto ni aliyekuwa Msimamizi wa uchaguzi huo James Magego, Mbunge wa Viti Maalumu, Jane Jerry na aliyekuwa Mwenyekiti wa uchaguzi huo ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Kisangi. (Picha na Christopher Lissa).
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Temeke, Lawama Mohamed akizungumza katika Mkutano Mkuu wa umoja huo, uliofanyika katika ukumbi wa Sabasaba,Dar es Salaam. |
Zifuatazo ni picha Wajumbe wakipiga kura👇
================================== |
Wasimamizi wakihesabu kura |
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇