LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 26, 2022

CCM YAANZA VIKAO VYA JUU VYA MCHUJO NA UTEUZI WA MWISHO KWA WALIOOMBA UONGOZI NGAZI YA WILAYA, LEO CC, KESHO NA KESHOKUTWA NEC

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Jumatatu, Septemba 26, 2022 kitaanza kufanyika vikao vya kawaida vya Uongozi ngazi ya Taifa Jijini Dodoma, ambapo leo kitafanyika Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC) na kesho na keshokutwa (tarehe 27 na 28 Septemba, 2022) Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi Komredi Shaka Hamdu Shaka, amesema, pamoja na mambo mengine vikao hivyo vitakuwa na kazi ya kupokea mapendekezo, kujadili, kupitisha na kufanya uteuzi wa mwisho wa wanachama ambao wameomba uongozi wa Chama katika ngazi ya wilaya.

"Vikao hivyo vilitanguliwa na Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, kilichofanyika tarehe 22 na 23 Septemba, 2022 Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI", amesema Komredi
Shaka Hamdu Shaka.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi Komredi Shaka Hamdu Shaka

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages