New York Marekani
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata
Mulamula amekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa
Mhe. Chrysoula Zacharopoulou katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja
wa Mataifa jijini New York.
Katika mazungumzo yao viongozi hao
wamejadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo na namna ya kuendelea
kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Ufaransa na namna ya
kuendeleza sekta za uchukuzi, muindombinu, kilimo, biashara na
uwekezaji nchini.
Viongozi hao pia wamejadiliana namna ya
kuongeza ujazo wa biashara kati ya Tanzania na Ufaransa na kuihusisha
sekta binafsi katika harakati za kuinua uchumi wa Tanzania.
Katika
tukio jingine Waziri Mulamula amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Rwanda Mhe. Vincent Biruta jijini New York na kujadiliana juu ya masuala
yenye maslahi baina ya nchi hizo.
Viongozi hao wajadili namna
wanavyoweza kushirikiana kupitia sekta ya biashara, uwekezaji na
uchukuzi na hivyo kuchangia harakati za ukuzaji wa uchumi wan chi hizo.
Viongozi
hao wako jijini New York kuhudhuria Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la
Umoja wa Mataifa (UNGA) unaoendelea nchini Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiangalia kitabu cha taarifa alichopatiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Chrysoula Zacharopoulou walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja wa Mataifa jijini New York.
Waziri Mulamula alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Mhe. Vincent Biruta jijini New York na kujadiliana juu ya masuala yenye maslahi baina ya nchi zao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇