LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 26, 2022

ABUBAKAR MLAWA ATWAA TENA UENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI BAGAMOYO

Na Scola Msewe, Bagamoyo

Mwanahabari mkongwe Abubakari Mlawa ameshinda tena Uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kwa kura 607 Kati ya kura 727 kwa Asilimia 83.47 ya kura zote kati ya Wagombea watatu.


Akitabgaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bagamoyo Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi mkuu CCM na jumuiya zake ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdallah alisema aliyemfuatia ni  Saumu Hoja  alipata kura 87  sawa na Asilimia 12.24 huku wa mwisho ni Hassan Shariff alipata kura 31 sawa na Asilimia 4.29.


Mlawa anaongoza jumuiya hiyo ya Wazazi Wilaya ya Bagamoyo kwa awamu ya pili sasa ambapo awamu ya kwanza alichaguliwa mwaka 2017 na Sasa anapata Tena ushindi wa kuongoza jumuhiya hiyo kwa kipindi cha pili.


Uchaguzi huo wa jumuiya ya Wazazi Wilaya Bagamoyo ulifanikiwa katika Ukumbi wa shule ya Sekondari Lugoba huko Chalinze na Wajumbe walioshiriki ni kutoka Katika Kata 25 za Wilaya nzima ya Bagamoyo yenye majinbo mawili ya uchaguzi ambayo ni Jimbo la Chalinze na Jimbo la Bagamoyo.


Kwa upande wa nafasi ya Wajumbe halmashauri kuu ya CCM Wilaya na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya walioshinda nafasi hiyo ni Tabia Nassoro kwa kupata kura 449.


aliyeshinda nafasi ya Wajumbe wa mkutano mkuu wa Wazazi mkoa kuwa ni Hussein Mramba aliyepata kura 267 huku nafasi ya Ujumbe wa mkutano mkuu wa CCM mkoa ikichukuliwa na Beatha Mchopa kwa kura 330.

Mlawa akipiga kura.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages