Na CCM Blog
Familia ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ally Hassan Mwinyi imeatangaza msiba mtoto wake Hassan Ally Mwinyi ambaye ni Pacha wa Rais wa Zanzibar wa sasa Dk. Hussein Mwinyi, Taarifa ya Afisa Habari M. A. Mlawa imesema msiba huo umetokea leo alfajiri.
Taarifa ya mazishi aliyotoa Mlawa, imesema Wanawake walikuwa Chukwaami, karibu na Skuli ya High View, kwa dua na sala saa 4 asubuhi na waliendelea Chukwani.
Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Saa 5 maiti iliondoka Chukwani kwenda Mangapwani ambapo Wanaume wamesali sala ya adhuhuri Mangapwani ambapo imepatapatikana sadaka iliyofuatiwa na visomo mpaka muda wa alasiri na baadaye Wanaume wamesalia maiti na kuzika baada ya sala ya alasiri Mangapwani.
Blog ya Taifa ya CCM, inatoa pole kwa Familia ya Mzee Mwinyi na kwa Rais Dk. Myinyi kwa kuondokea na Pacha wake.إنالله وإناإليه راجعون -Ina Lilah Waina Ilayh r'ajiuun.
Hassan Ally Mwinyi enzi za uhai wake. |
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇