Zanzibar.
Pacha wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, Hassan Ali Hassan Mwinyi amezikwa leo Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Maziko hayo ya Hassan Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia leo alfajiri, yameongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi.
Pia Rais mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaji Ali Hassan Mwinyi, ambaye ni Baba mzazi wa Marehemu, aneshiriki kikamilifu katika maziko hayo.
Wengine waliohudhuria ni viongozi mbalimbali wa Dini, Siasa, Serikali na wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇