LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 17, 2022

CHELSEA STARWAY GROUP, YAWAPIGA MSASA WAFANYAKAZI WAKE

Na Jumanne Gude

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Chelsea Starway Group, Martin Mbwana, amewataka wafanyakazi wa kampuni hiyo kuzingatia mafunzo waliyopata ya kuwajengea uwezo katika majukumu yao.


Martni alitoa wito huo wakati wa kufunga mafunzo hayo, yaliyofanyika katika ofisi ya kampuni hiyo, Dar es Salaam.


Amesema mafunzo hayo ni muhimu sana, ambayo yatawajenga katika kutimiza majukumu yao ya kuwahudumia wateja wao.


Pia Martin amesema wachape kazi ili wafikie malengo waliyojiwekea kwa maslai ya pamoja na  kampuni.


Amesema waongeze upendo miongoni mwao, pia, wapende kazi zao na kwamba waendelee kufanyakazi hata kama kuna mabadiliko katika kampuni hiyo.


"Kutakuwa na mabadiliko katika utendaji kazi, msiogope lengo ni kuhakikisha kampuni yetu inakuwa kubwa na kuyafikia malengo yetu, kwahiyo ongezeni upendo", amesema.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Starway Group, Martin Mbwana, akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo waliohitomu mafunzo ya kuwajengea uwezo katika kazi zao, akifunga mafunzo hayo, Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Community Health & Development Initiative (CHDI), Eugen Mikongoti, akizungumza na  wafanyakazi wa kampuni hiyo waliohitomu mafunzo ya kuwajengea uwezo katika kazi zao, akifunga mafunzo hayo, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Starway Group, Martin Mbwana na Mkurugenzi Mtendaji wa Community Health & Development Initiative (CHDI), Eugen Mikongoti, wakiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu (Picha zote na Jumanne Gude).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages