Na Mwandishi Maalum, Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi jana Jumanne alikuwa na kikao na Viongozi kutoka Wizara na Taasisi ambazo kwa namna moja ama nyingine, zinahusika na masuala ya uwekezaji.
Mhe. Mwanasheria Mkuu aliitisha kikao hicho kufuatia uwepo wa changamoto na malalamiko kutoka kwa baadhi ya watu wanaotaka kuwekeza nchini.
Baadhi ya changamoto hizo au malalamiko hayo ni kuhusu utendaji wa Taasisi za Serikali, wimbi kubwa la migogoro ya uwekezaji katika mabaraza ya usuluhishi ya Kimataifa pamoja na kukosekana kwa utaratibu mzuri wa pamoja katika kushughulikia changamoto hizo.
Kikao hicho cha siku moja na ambacho pia kilihudhuriwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa kililenga kuzijadili changamoto hizo pamoja na namna bora ya kuzishughulikia.
Wizara na Taasisi zilizohudhuria kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtumba Dodoma ni Ofisi ya Rais Ikulu, Wizara ya Fedha na Mipango, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Katiba na Sheria.
Taasisi nyingine zilizoshiriki kikao hicho ni Kituo cha Uwekezaji ( TIC) na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Uwekezaji wa Mauzo ya Nje (EPZA) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dk. Eliezer Feleshi akifungua kikao alichokiitisha kuhusu masuala ya uwekezaji nchini. kikao hicho kilihusisha viongozi ambao Wizara ama Taasisi zao zinazohusika na Masuala ya Uwekezaji. Kikaoini kilifanyika siku ya jumanne katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtumba Dodoma
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇