LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 20, 2022

WANANCHI KUTOKA VISIWA 8 MKOANI KAGERA KUNUFAIKA NA UMEME MWAKA WA FEDHA 2022/2023.



Na, Lydia Lugakila 

Kagera.


Serikali kupitia Wizara ya nishati imesema katika mwaka huu wa fedha 2022/23 Kati ya visiwa 35 vinavyopatikana katika ziwa Victoria kwa mkoa wa kagera visiwa takribani 8 vinatarajia kupokea umeme kutoka katika grid ya taifa.


Akizungumza na wananchi katika mkutano wa adhara  uliofanyika  katika Kijiji Cha Bukoki kitongoji Nshambya kata Muhutwe wilaya ya Muleba Mkoani Kagera waziri wa nishati  January Makamba amesema kuwa serikali inapambana ili kuhakikisha inawapatia wananchi waishio visiwani umeme wa uhakika kwa kuanzia baada ya mradi wa kufua umeme wa Rusumo kukamilika  na miradi mingine ndani ya mkoa wa Kagera.


Aidha amewataka wananchi kuendelea kutunza miradi na miundombinu ya umeme inayojengwa kwani ndiyo chanzo kikuu cha kuwapatia umeme na kuwaondoa wasiwasi wananchi wa visiwani juu ya kutumia gharama kubwa ya kununua unit moja ya umeme kwa wawekezaji ambapo kwa Muleba kusini vitapata visiwa 4 na Muleba kaskazini visiwa vinne.



Pia  waziri Makamba  ametembelea mradi mwingine uliopo kata ya Bureza wilaya ya Muleba  ikiwa Ni kituo cha kupozea umeme ambapo meneja wa Tanesco wilaya ya Muleba mhandisi Lameck Said amesema kuwa kituo hicho kwa mwaka huu wa fedha 2022/23 kitagharimu shilingi bilioni 8 ikiwa mpaka Sasa mradi umekamilika kwa asilimia 49.8.


"Kwa mwaka wa fedha 2021/22 tulipokea shilingi Bilioni 2 na mwaka huu wa fedha tumepokea Bilion 6 lengo la kujenga laini hii ya umeme ni kupunguza nguvu kubwa kutoka katika kituo cha kupozea umeme Kibeta  ambapo laini hii itagawa umeme maeneo ya Kamachumu, Muleba mjini pamoja na Ujenzi wa bomba la mafuta  jambo litakalopelekea kupunguza adha ya kukatika katika kwa umeme" Alisema mhandisi Said.


Kwa upande mwingine waziri Makamba ametembelea mradi mwingine wa Geita Nyakanazi Substation uliopo wilaya ya Biharamulo maeneo ya Nyakanazi ambapo ametaja  kulidhishwa na Ujenzi wa mradi huo.


Naye kaimu meneja miradi usafirishaji na usambaji Tanesco mhandisi Frank Mashalo amesema mradi wa Nyakanazi baada ya kukamilika utasaidia kuondoa adha ya umeme katika mikoa mitatu ikiwemo Kagera,Geita na Kigoma  ambapo mpaka Sasa kituo hicho kimefungwa transfoma 2 zenye uwezo wa kugawa katika mikoa hiyo.


" Maeneo ya Kagera yatakayonufaika na mradi wa kituo cha Nyakanazi ni pamoja na Biharamulo,Ngara na maeneo mengi jambo ambalo litasaidia Kagera kuondokana na umeme wa Uganda na kuanza kutumia grid ya taifa ambapo amesema mradi huo unajengwa na kampuni ya LARSEN & TOUBRO chini ya mkandarasi ndg. Rajeev Nsomvesh" Alisema  mhandisi Mashalo. 


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages