LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 16, 2022

WABUNGE MAGANGA, CHEREHANI WAFANYA MKUTANO WA PAMOJA MBOGWE



MAGANGA Mbunge wa Jimbo la Mbogwe ametembelewa na  Mhe Chelehani Mbunge wa Jimbo la ushetu wakati wa ziara yake kwenye Jimbo la Mbogwe.


Mhe Mbunge akiambatana na Watalaamu toka Halmashauri wakiongozwa na Kaimu DED Mr King ametowa siku 15 Stendi ndogo ya idarafuma ianze kutumika kama ilivo matakwa ya wananchi 15-30/07/2022 ili trekita zote za Mjini zipaki maeneo hayo kuepusha ajari za barabarani za kila Mara.


Pia Maganga amemuagiza Meneja TARURA Mbogwe kukaa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbogwe kutatuwa Tatizo la Majina ya vibao vya Postikodi na kufuata Majina yaliyopendekezwa na vikao kuanzia Kijiji na WODC Mbalimbali na pia yeye amesha zungumuza na Mhe Waziri wa Mawasiliano na teknolojia ya habari comrade Nape Nnauye.


Pia Mbunge amefafanua kuwa kwasasa Mbogwe tuna Mamulaka ya Maji Mbogwe (GEWASA) Mhe Waziri-AWESO  ametimiza ahadi yake kwa wana Mbogwe, Maana tumepata GN 775 ,Lakini amemuagiza Meneja RUWASA na GEWASA Kushughulikia Malalamiko ya bei kupanda .


Mhe CHELEHANI alisema hongereni sana Mbogwe Maganga anapambana 2022/2023 upembuzi yakinifu wa Maji ya ziwa Victoria unaendelea na Mtapata Maji hayo, Lakini pia Barabara ya Mwabomba-Masumbwe ushetu -to Mbogwe iko TANROADS na imetengewa Zaidi ya Bilioni 1.356 kwajili ya kiwango cha lami 124 KM na Daraja la 700 Milioni 


Mhe CHELEHANI amesema jimbo la Mbogwe bajeti ya 2022/2023 Mumepewa bilioni Tisa (9) na Mhe Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN.


MWISHO: Mhe MAGANGA Alimushukuru Mhe CHELEHANI kwa kutembelea Jimbo la Mbogwe na kuwaomba wananchi kujitokeza tarehe 23.08.2022 kwaajili ya sensa ya watu na Makazi na 


akarudia kumupongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe Bi SAADA na timu nzima ya Madiwani  kwa kupandisha Mapato toka Milioni 900 Mpaka bilioni tatu na kuwaomba tuzidi kumuunga Mkono Mhe Rais SAMIA SULUHU HASSAN



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages