LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 27, 2022

SH. BILIONI 8 ZA MRADI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI IRAMBA KUNUFAISHA WANAKIJIJI CHA MSIMBA WILANI HUMO

Na Hemedi Munga, Iramba.

Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda amewataka wananchi wa kijiji cha Masimba kujiandaa kwa kupima mashamba na kujisajili kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo cha umwagiliaji kitakachogharimu takribani Tsh 8 bilioni mwaka wa fedha 2022/2023.


Mwenda ametangaza neema hiyo leo Julai 26, 2022 wakati alipofanya ziara katika kijiji cha Masimba wilayani hapa.


Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika kijiji hichi ili kuendelea kuwawezesha wananchi katika shughuli za kiuchumi, hatimaye kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.


‘’ Hapa Masimba tuna bwawa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, hivyo tunatarajia kupokea Tsh 8 bilioni kwa ajili ya kuboresha na kutengeneza mifereji, kuweka kingo vizuri zisijae maji na kusafisha mashamba.’’ Alisama


Aidha, alithibitisha kuwa fedha hiyo tayari imeishapitishwa katika bajeti ya mwaka huu, hivyo itakuja ni lazima tufanye maandalizi ya mradi huo mkubwa katika wilaya yetu.


‘’ Sisi wananchi tujiandae kuzipokea hizi fedha na kuzisimamia vyema ili zifanye kazi ambayo Rais Samia ameikusudia.’’


Tunaamini kuwa fedha hii itaboresha na kujenga miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji, dhana za kisasa, kutafuta masoko na uzalishaji wa mbolea.


Nasisi wasaidizi wa Rais Samia tunao wajibu wa kuja kuwahimiza wananchi kupokea mrejesho wa fedha hizi ambazo serikali imeitenga kwa lengo la kuboresha miundombinu mbalimbali ili kukuza tija ya kilimo kwa wakulima pamoja na kuongeza uzajilishaji na uchumi wa nchi ya Tanzania.


Halikadhalika, aliseama serikali itajenga ghala la kisasa hapa Masimba kwa ajili ya kuhifadhia mazao kwa sababu wanaamini kuwa uzalishaji utakuwa mwingi.


Kufuatia uwekezaji huo, Mwenda amewataka wananchi hao kuhakikisha wanasajiliwa ili wafahamike kwa sababu serikali imekusudia kuwawezesha walime kilimo cha kisasa kwa kuwapa mbegu bora na kuwaleta wataalamu watakaopima udongo ili kubaini aina ya mbegu na mbolea itakayotumika katika eneo hilo.


‘’ Ni hakika mbegu zinamea tofauti kulingana na ardhi inayotumika, hivyo wataalamu wanakuja kupima udongo ili kutengeneza mazingira rafiki ya uzalishaji wenye faida.’’  Alisema na kuongeza kuwa


‘’Nilazima mjipange ili muende sawa na mipango ya serikali ili kwa pamoja tuboreshe uchumi wa mtu mmoja mmoja na sisi tunaoongoza, tuongoze wilaya yenye wananchi ambao mmekula, mmeshiba na uchumi wenu upo vizuri.’’


Hali hii itaendelea kuhakikisha kuwa nchi hii inakuwa na utulivu, amani na watu wake wanaishi kwa upendo.


Katika hatua nyingine, Mwenda aliwataka wananchi hao kutunza chakula kwa sababu msimu huu unadaiwa kutokuwa mzuri hasa kwa baadhi ya wakulima.


‘’ Ninawaomba ndugu zangu hifadhini chakula ili kitusaidie hapo baadae na mtakapouza mpate bei iliyokuwa nzuri.’’


Akiongea katika mkutano huo Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika wilayani hapa, Marietha Kasongo aliwataka wakulima hao kuchangamkia fursa hii ili kulima kwa tija katika kilimo cha umwagiliaji chenye uhakika kwa kuvuna.


‘’ Tambueni ndugu zangu wakulima kulima kwenu ndiko kunanifanya mie niwepo, hivyo limeni kwa tija.’’


Kwa upande wake Diwani wa kata ya Urughu wilayani hapa, Simion Tyosela alisema kuwa wao wamejiandaa kuopokea mradi huo wakiamni sasa wanakwenda kulima kilimo endelevu wakati wa masika na kiangazi.


‘’ Tunamshukuru sana Rais Samia kwa sababu maisha ya wananchi wa Masimba yamepata neema, kubalidilka na kupata uchumi mkubwa.’’


Aidha, aliwataka wananchi hao kuutumia mradi huo ipasavyo ili uwabadilishe maisha yao.


Mradi huo itakuwa ni sababu ya kupata pumba zakutosha kutokana na kilimo cha mpunga ambapo kitawawezesha wananchi kuchoma tofali na kujenga nyumba bora za kisasa huku wakiutumia umeme kuweka mashine za kukoboa mpunga.


Halikadhalika, Tyosela alisema kuwa uchumi huo utawawezesha wananchi kusomesha watoto wao katika shule mbalimbali zikiwemo za serikali na binafsi.


Naye Ramadhani Bundala alimshukuru Mkuu huyo wa wilaya kwa kuwaletea neema katika kijiji chao nakuomba mradi huo uwahi kufika.


Abdi Bakari alimshukuru na kumuombea afya njema Rais Samia kwa kuwakumbuka kuwaletea mradi mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji.


‘’ Ni kama neema ambayo imetushukia hapa, mradi wa Tsh 8 bilioni tumeletewa hapa, hakika najisikia faraja nakuwa tayari kuupokea mradi huu kwa shangwe na furaha.’’


Naye Ramadhani Magingi mmoja wa mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika kijiji hicho alisema kuwa kijiji chao kinakwenda kuwa juu huku akifafananisha maendeleo watakayo yapata huwenda yakawa ni zaida ya wananchi wa Mwanzugi wilayani Igunga Mkoa wa Tabora.


Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda akiwataka wananchi wa kijiji cha Masimba wilayani Iramba kujiandaa na uwekezaji wa bilioni nane kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji katika kijiji cha Masimba leo Julai 26, 2022. Picha na Hemedi Munga



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages