LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 27, 2022

MBUNGE DK. DOROTHY KILAVE APOKEA VIFAA TOKA NMB KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU KATIKA SHULE NNE JIMBO LA TEMEKE

Temeke, Dar es Salaam

Mbunge wa Jimbo la Temeke Mhe. Dk. Dorothy Kilave, amepokea vifaa vya mabati 600, viti, meza na madawati viliyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili kuchangia uboreshaji wa Miundombinu ya elimu katika Jimbo la Temeke, Dar es Salaam.


Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge Jimbo la Temeke, na kuifikia Blog ya Taifa ya CCM (CCM Blo), imesema, NMB imetoa chango wa vifaa hivyo kupitia Kampeni ya Boresha Vya Kale iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ya Mbunge Jimbo hilo la Temeke.


Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, makabidhiano ya Vifaa hivyo yalifanyika juzi Julau 25, 2022, katika hafla iliyofanyika Shule ya Sekondari Kibasila, na Mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Tawala  wa Mkoa wa Dar es Salaam Hassan Rugwa.


Taarifa imesema, Katibu Tawala huyo alimpongeza sana Mbunge wa Temeke Dk. Dorothy Kilave kwa ubunifu katika utatuzi wa kero za Wananchi.


Pamoja na Katibu Tawala huyo, hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Abdallah Mtinika, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Madiwani wa Jimbo la Temeke na Wajumbe wa Mfuko wa Jimbo hilo.


Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe Dk. Dorothy Kilave amewashukuru Benki ya NMB kwa mchango huo, na akaendelea kukaribisha Wadau wengine ndani na nje ya Jimbo kuendelea kuchangia vifaa Kwa ajili ya kuboresha Elimu Jimbo la Temeke akisema Kampeni hiyo ni endelevu.


Kwa upande wake Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, aliahidi kuwa Benki hiyo itaendelea kutia ushirikiano zaidi kwa ajili ya Maendeleo ya Jimbo  na Wilaya ya Temeke kwa Ujumla.

Mbunge wa Jimbo la Temeke Dk. Dorothy Kilave akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa vifaa na Benki ya NMB, juzi

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages