LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 31, 2022

PROF. NDAKIDEMI AUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA KUHAMASISHA SENSA MOSHI VIJIJINI

Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro, Prof. Patrick Ndakidemi ameamua kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika Kampeni ya kuhamasisha wananchi kushiriki kwa wingi katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika nchini kote Agosti 23, mwaka huu.

Prof. Ndakidemi alishiriki katika mkutano wa hadhara Julai 29, 2022 katika Kijiji Cha Shimbwe Juu Kata ya Uru Shimbwe Jimboni kwake ambapo alihamasisha wananchi wakitokeza kwa wingi na kuhesabiwa siku ya Sensa tarehe 23.8.2022. 

Wananchi walijitokeza kwa wingi kumsikiliza mbunge. Baada ya mkutano aligawa vipeperushi kwa wananchi vinavyoelezea umuhimu wa sensa kuwaletea maendeleo.



Prof. Ndakidemi (katikati) akiwa pamoja na wananchi wenye furaha baada ya kuwagawiwa vipeperushi vyenye ujumbe wa Sensa.


 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages