LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 14, 2022

MWENYEKITI WA CCM RAIS SAMIA AOMBOLEZA KIFO CHA MBUNGE ZA ZAMANI WA CHAMA CHA CUF

CCM HQ, Dodoma

Chama Cha Mapinduzi Kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa zamani wa Chama Cha Wananchi (CUF) na Mkurugenzi wa Fedha na Mipango Khadija Makontena kilichotokea leo Alhamisi 14 Julai, 2022.


Taarifa iliyotolewa Katibu Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka imesema  kufuatia kifo hicho, Mwenyekiti wa CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu  Hassan amemtumia salaam za pole Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF ) Profesa Ibrahim Lipumba, familia, ndugu na jamaa.


“Bi Khadija tokea kuanzishwa mfumo  wa Vyama Vingi vya siasa amekuwa akishiriki kikamilifu  katika uwanja wa  siasa za ndani na nje ya  chama chake huku  akiamini   siasa za umoja na maelewano.


Mwenyezi Mungu awape ustahamilivu na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.


Sisi Sote niwa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea", amesema Mwenyekiti wa CCM Rais Samia.

Mwenyekiti wa CCM Rais Samia

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages