Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro (Aliyeshika Bendera ya Taifa) akiwa na timu
ya Taifa ya Riadha pamoja na mwanariadha Alphonce Felix Simbu baada ya
kushinda medali ya Fedha kwa kuibuka mshindi wa pili mbio za marathon
katika Michezo ya Jumuiya ya Madola jijini Birmingham, Uingereza, nyuma
ya Victor Kiplagat wa Uganda leo. Mkimbiaji Hamisi Misai (wa tatu
kulia) alimaliza katika kumi bora ya mashindano hayo kwa kushika nafasi
ya nane. Wa pili kutoka kushoto ni Failuna Matanga ambaye alimaliza mtu
wa tano katika marathon ya wanawake wakati Jackline Sakilu (wa pili
kulia) akimaliza mwishoni akichechemea kutokana na maumivu ya msuli
aliyoyapata akiwa kilomita 17 tu ya mchuano huo. Hivyo alichechemea hadi
akamaliza huku akishangiliwa sana na umati mkubwa wa watu uliokuwepo.
Kushoto ni kocha mkuu Suleiman Nyambui na kulia ni kocha msaidizi Lwiza
John. (Picha zote na Mpigapicha Maalum).
|
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇