LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 21, 2022

'MASIKINI' MANARA AFUNGIWA NA TFF MIAKA MIWILI

 MANARA


Maamuzi ya kufungiwa kwa Manara yametangazwa leo Alhamis (Julai 21), na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ katika mkutano na Waandishi wa Habari.

Kamati ya Maadili ya TFF imebaini Haji alitumia Lugha ya vitisho dhidi ya Rais wa Shirikisho Wallace Karia wakati wa mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ kati ya Young Africans dhidi ya Coastal Union uliopigwa Julai 02 jijini Arusha, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.


“Wewe unanifuatilia sana na hii ni mara ya tatu, hunifanyi lolote, huna uwezo wa kunifanya lolote.” Kauli ya Manara ambayo inadaiwa aliitoa dhidi ya Rais Karia.

Msemaji wa Klabu ya Young Africans Haji Sunday Ramadhan Manara, amefungiwa kujihusisha na Mpira wa Miguu (Soka), Kwa kipindi Cha Miaka miwili na faini ya Shilingi Milioni 20.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages