LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 26, 2022

KINANA AWATAKA VIONGOZI NA WATENDAJI KUONDOA VIKWAZO KATIKA SHUGHULI ZA WANANCHI, ASEMA SEKTA BINAFSI INAAZA NA WATU WA KAWAIDA

Nkasi, leo
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana amewataka viongozi na watendaji wa serikali kuhakikisha wanarahisisha ufanyaji wa shughuli za wananchi kwa kuwaondolea vikwazo kwa kuwa sekta binafsi inaanza na wao.

Kinana ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo la Nkasi Kaskazini eneo la Lyazumbi wakati wa mapokezi ya kuanza ziara mkoani Rukwa akitokea mkoa wa Katavi.

"Serikali inafanya jitihada za kuimarisha na kuboresha mazingira ya sekta binafsi nchini ili ifanye vizuri, sasa sekta binafsi inaanza na wananchi wa kawaida. Tuwaondolee kero wananchi wetu na tuwarahisishie kufanya shughuli zao iwe ni wakulima, wafugaji, bodaboda, wamachinga au wafanyabishara." Amesema Kinana

Akimkaribisha mkoani Rukwa Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Ndugu Rainer Lukalah
amemueleza Ndg Kinana kuwa hali ya siasa katika mkoa huo ni shwari na wanaridhishwa na kazi kubwa ya maendeleo inayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kinana ameingia mkoani Rukwa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya uimarishaji chama na ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka.

Makamu Mwenyekikiti wa CCM Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akipokea saluti kutoka kwa Vijana wa UVCCM baada ya Vijana hao kimvisha skafu, wakati akipokewa katika eneo la Lyazumbi Jimbo la Nkasi Kaskazini, kuanza ziara mkoani Rukwa akitokea mkoa wa Katavi, leo. Kushoto ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka. Zifuatazo ni picha mbalimbali Kinana akiingia mkoani Rukwa👇


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages