LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 26, 2022

MAANDALIZI KAMPENI YA UHAMASISHAJI SENSA YAPAMBA MOTO MUSOMA VIJIJINI



 JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI -  KAMPENI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI


KAMPENI hiyo itafanywa ndani ya Kata zote 21 zenye Vijiji 68.


MUDA wa KAMPENI

Kuanzia tarehe 30.7.2022 hadi tarehe 22.8.2022


UZINDUZI

*Jumamosi, 30.7.2022

*Saa 9 Alasiri

*Kijijini Busekera


VIONGOZI watakaongoza Kampeni hiyo ni:


*Mkuu wa Wilaya

(Dkt Khalifan Haule)


*Mkurugenzi wa Halmashauri

(Ndg Msongela Palela)


*Mbunge wa Jimbo

(Prof Sospeter Muhongo)


VIKUNDI VYA UHAMASISHAJI vimetayarishwa na Mbunge wa Jimbo. Vikundi hivyo ni:


*Kwaya ya Bugoji

*Kwaya ya Kiriba


*Ngoma ya Liranda Bugwema

*Ngoma ya Kiwanjuki Kiriba

*Ngoma ya Mbegete Nyakatende


*Mtelezo Show ya Nyakatende


KIPEPERUSHI kimoja chenye kurasa/pande mbili (kimeambatanishwa hapa) kitagawiwa ndani ya Vijiji vyote 68.


JIANDAE KUHESABIWA

 Tarehe 23.8.2022


Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:

www.musomavijijini.or.tz


Ofisi ya Mbunge

Jimbo la Musoma Vijijini

www.musomavijijini.or.tz


Tarehe:

Jumanne, 26.7.2022

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages