Wananchi wa Kijiji cha Chiwondo, wilayani Chamwino, Dodoma wameeleza furaha yao kwa kuishukuru serikali kuteua Kijiji chao kuwekwa kwenye mpango wa kurasimisha ardhi yao utakaofanywa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge nchini (MKURABITA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma.
Urasimishaji huo unaoongozwa na Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa MKURABITA, Anthony Temu utafanyika kwa siku 12, katika kijiji hicho chenye vitongoji 8 ambavyo ni; Kawawa, Karume, Matanga, Ngutoto, Mkokani, Majengo, Chapakazi na Chikwama.
Meneja wa Urasimishaji Ardhi Vijijini wa MKURABITA, Anthony Temu akielezea kuhusu mpango huo katika kikao cha Halamashauri ya Kijiji hicho pamoja na maafisa wa Halamashauri ya wilaya hiyo.
Baadhi ya maafisa wa Hamashauri wakiwa katika kikao hicho cha maandalizi.Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Anthony Temu akielezea kuhusu mpango huo wa urasimishaji ardhi na wananchi wakielezea furaha yao...
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇