LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 12, 2022

KAGUO: BILA RUZUKU YA BILIONI 100 RAIS BEI YA MAFUTA INGEPAA ZAIDI+video

 Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Titus Kaguo ameomba watanzania kuacha tabia ya kukejeli ruzuku ya sh. bilioni 100 inayotolewa kila mwezi na Rais Samia Suluhu Hassan kuweka unafuu kwenye bei ya mafuta nchini, kwamba haijasaidi.

Amesema si kweli bali kinachotakiwa ni kumuunga mkono Rais kwa wema na huruma aliyonao kwa watanzania kutoa ruzuku hiyo ambayo imesaidia sana kupunguza bei ya mafuta kwani bila ruzuku iyo mafuta kwa sasa yangeuzwa zaidi ya sh. 3600 kwa lita kwa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoani ingekuwa bei mbaya zaidi.

Kaguo (wa pili kulia) akifafanua jambo mbele ya wageni waliotembelea Banda la Ewura katika Maonesho ya Biashara ya 46 jijini Dar es Salaam Julai 10, 2022.

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Kaguo akielezea manufaa ya Ruzuku hiyo inayotolewa kwenye mafuta na Rais Samia.....


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages