LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 11, 2022

JICA YAONYESHA NIA YA KUSHIRIKIANA NA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI (AG)

Na Mwandishi Maalumu, Ofisi ya SG, Dodoma
Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani ( JICA) limeelezea nia yake ya kutaka kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) katika maeneo mbalimbali.

Nia hiyo ya JICA, imeelezwa leo Jumatatu, Julai 11, 2022 na Mwakilishi wa JICA Ofisi ya Tanzania Bw. Asano Siezaburo, alipokutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Onorius Njole, katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mji wa Serikali wa Mtumba, Jijini Dodoma.

“ Tumekuja tujadiliane na kuona ni maeneo gani Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inaweza kunufaika na misaada inayotolewa na JICA, hii ni kwa sababu tunataka kuwa na  ushirikiano na Ofisi hii”.  akasema  Bw. Seizaburo aliyekuwa ameambatana na Bi. Yukiko  Karanuki katika mazungumzo hayo.

Moja ya eneo ambalo JICA imeonyesha nia  ya kutaka kusaidia ni katika la kujenga uwezo ( Capacity Building)  kwa Mawakili wa Serikali.

Kwa kuanzia JICA itatoa fursa kwa Mawakili watatu (3 ) kwenda kujengewa uwezo kwa kuwapatia mafunzo katika eneo la Sheria za Biashara.

Ujumbe huo wa JICA umeitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuainisha maeneo mengine ya ushirikiano na kisha kuwasilisha JICA kwa majadiliano zaidi.

Kwa upande wake Kaimu Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Njole ameishukuru JICA kwa   kuona umuhimu wa kutaka kuwa na ushirikiano na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akasema, huduma za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni mtambuka na zinazogusa kila sekta ya nchi hii na kwa sababu hiyo  nia hiyo ya JICA ya kutaka kuwa na mahusianao na OMMS ni muhimu sana.

“Karibu katika kila misaada ambayo JICA  inatoa hapa Nchini iwe TANESCO kama ulivyosema, katika Sekta  yoyote ile, kuna mkono wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na hili halikwepeki kwa hiyo kila mnapotoa ushirikiano katika  sekta fulani basi muikumbuke Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mmefanya  vema kuona umuhimu wa Taasisi hizi mbili kuwa na  majadiliano ya kuona namna gani tunaweza  kushirikiana”. amesisitiza Bw. Onorius Njoel ambeye pia ni Mwandishi Mkuu wa Sheria.

Aidha  Kaimu Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali  ameishukuru JICA pia kwa kutoa fursa ya kuwajengea uwezo Mawakili wa Serikali  katika  eneo la  Sheria za Biashara na kwamba  mwanzo huo ni  mzuri.

Akaahidi kwamba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  itaangalia maeneo mengine ya ushirikinao
Katika  mazungumo hayo, Kaimu Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliambatana na  Bi. Slyvia Matiku  Mkurugenzi Msaidizi Divisheni ya  Uratibu na Huduma za Kisheria na  Bw. Sunday Hyera Mkurugenzi Msaidizi  Divisheni ya Mikataba.

Ujumbe wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ulioongozwa na Kaimu Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Bw. Onorius Njole katika mazungumzo na Ujumbe wa JICA Ofisi ya Tanzania, uliogozwa na Bw. Asano  Siezaburo.  Majadiliano hayo  yalilenga  kuangalia  namna Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inavyoweza kunufaika na misaada ya JICA. Wengine katika picha ni  Bi. Slyvia Matiku ( OMMS) Bw. Sunday Hyera ( OMMS) na  Bi. Yukiko  Karanuki  JICA Tanzania (Na Mpigapicha Maalum).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages