LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 1, 2022

WAZIRI MKUU MAJALIWA AAHIDI WATUMISHI LINDI KUTEKELEZA MAAGIZO YALIYOTOLEWA NA MWENEZI WA CCM SHAKA

Na Mwandishi Maalum, Lindi
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameahidi kuwa maagizo na maelekezo yote yaliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa(NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka yatatekelezwa na watumishi wote wa umma mkoa wa Lindi.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara ya Shaka kwenye Mkoa wa Lindi aliyoifanya kwa siku nne, Waziri Mkuu amesema yote ambayo yameelezwa yatafanyiwa kazi na hakuna hata agizo hata moja ambalo halitatekelezwa huku akitumia nafasi hiyo kueleza wana Lindi wamefurahishwa na ziara hiyo ya Mjumbe wa NEC.

“Umekutana na wananchi wa Mkoa wa Lindi, umetembelea miradi ya maendeleo , sisi wana Lindi tumefurahi sana kupata taarifa ya mafanikio ambayo yamepatikana, umewapongeza watumishi wa umma, nataka kukuhakikishia nami nilifanya ziara kwenye wilaya zote za mkoa huu, nimepata kutembelea miradi.

“Ulichokiona wewe  nami ndicho nilichokiona watumishi hawa ndio wanaotekeleza miradi hiyo. Mkoa wa Lindi kuna mabadiliko na hizi ni jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi kupitia Serikali yetu inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan,”amesema  Waziri Mkuu.

Amefafanua taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM imeeleza kwa kina mafanikio yaliyopatikana kwenye Mkoa wa Lindi na kueleza katika miudombinu ya barabara, tayari Serikali imeweka mipango ya kujenga barabara mbalimbali za mkoa huo.

“Barabara zetu za Mkoa huu wa Lindi ikiwemo ya Masasi, Nachingwea mpaka Liwale imeshaingia kwenye mpango wa utafutaji fedha na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ameshaiweka kwenye mipango ya ujenzi , hivyo kinachosubiriwa ni kupata fedha.

“Umezungumzia kuhusu Wanyamapori nami nimepokea, Mbunge wa Nchingwea Dk.Amandus Chinguile alikuja mezani kwangu  bungeni kunieleza, nilimuagiza Waziri apite huku Liwale, Nachingwea pamoja na maeneo mengine ya Lindi hadi kule maeneo ya Milola, Naibu Waziri alikuja amepita na ameona.

“Tunakwenda kuona idadi ya mifugo iliyoingia Selous idhibitiwe ili tembo warudi, tembo hawakubali kuchanganyika na mifumo mingine, hivyo tembo wale wanasogea hukuSerikali itasimamia hili na bahati nzuri Naibu Waziri alikuja na akaongazana na mbunge wa Nachingwe, hivyo tutahakikisha tunatekeleza maagizo yako ili kudhibiti wanyampori ambao wanakuja kwenye maeneo ya watu,”amesema Waziri Mkuu.

Kuhusu fidia kwa walioathirwa na tembo malipo yao yanaendelea kujadiliwa na wanaostahili kupata fidia kutokana na athari ambazo wamezipata kutokana na tembo hao zitawafikia.

“Katika Bunge hili la Bajeti Wizara ya Maliasili na Utalii itasoma bajeti yake na hili la fidia litakuwepo , hivyo wanaostahili fidia watalipwa,’amesisitiza Waziri Mkuu alipokuea akielezea namna watavyotekeleza maagizo ya Shaka kuhusu Serikali kuchukua hatua kukabiliana na wanyamapori.

Kuhusu bei ya mazao mbalimbali likiwemo zao la Ufuta, Waziri mkuu amesema Serikali imefanya utaratibu mzuri wa kupanga bei na hivi sasa wameshuhudia bei mpya kwenye mazao ikianza kunufaisha wakulima wa nchi hii akitoa mfano kuwa wakulima wa Namtumbo wameanza kunufaika na mfumo huu unatokana na utaratibu wa stakabadhi ghalani ingawa wakati unaanza kuna watu waliupinga na kuna baadhi ya wanasisa waligeuza kuwa ni suala la kisiasa.

Akizungumzia agizo la Shaka la kuitaka Serikali kuangalia namna ya kupunguza makato ya ushuru kwenye zao la ufuta ili wakulima wanufaike , Waziri Mkuu amesema agizo hilo watalifanyia kazi na tayari Rais Samia Suluhu Hassan ameshampa jukuku la kupitia makato na ameanza kuzunguka kila mkoa kwenye zao ambalo linanufaisha wakulima.

“Napita  kuangalia makato, ninyi ni mashahidi nilipokuwa kagera kulikuwa kuna makato 47 lakini tumeyapunguza.Serikali inataka kuona mkulima huyu anayevuja jasho ananufaika na kilimo, hivyo suala la makato tunalifanyia kazi na hakuna mzaha kwenye hili,”amesema.

Awali akizungumza wakati wa majumuisho hayo, Shaka ameeleza kwa kina kuhusu mafanikio ambayo ameyashuhudia kwenye Mkoa wa Lindi na hiyo imetokana na upendo mkubwa alionao Rais Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wa Lindi na watanzania kwa ujumla

“Katika Mkoa wa Lindi nimepita kila mahali kunajengwa, barabara zinajengwa, vituo vya afya, shule na majengo mengine ya huduma za kijamii yanaendelea kujengwa .Serikali imetoa zaidi ya Sh.bilioni 52 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo,”amesema Shaka.

Aidha amesema pamoja na mafanikio ya mkoa huo, bado kuna changamoto ya wanyamapori hata tembo kuvamia makazi ya watu na mashamba na hivyo kuleta athari zikiwemo za kujeruhi watu na kusabisha vifo .Pia wanyamapori hao wameharibu mazao ya wakulima na kuna uwezakano mkubwa kukawa na njaa, hivyo ameitaka Serikali kuchukua hatua kukabiliana na tembo hao.

Pia Shaka ametoa maelekezo kwa Serikali kuangalia namna ya kupunguza ushuru katika mazao kwani pamoja na bei ya ufuta kuongezeka kutoka Sh.2100 hadi Sh.2900 lakini mkulima hapati fedha yote hiyo kwasababu ya makato ya  ushuru yaliyopo, hivyo ni vema Serikali ingaalie namna ya kupunguza ili wakulima wanufaike.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka na Mbunge wa Ruangwa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakifurahia jambo wakati wakizungumza, wakati wa Mkutano wa majumuisho ya ziara ya Shaka mkoani Lindi, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Ualimu Nachingwea mkoani humo, leo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages