LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 1, 2022

UWT DAR WAMPA KONGOLE RAIS SAMIA KWA UTENDAJI KAZI ULIOTUKUKA, WASEMA AMEAMSHA ARI YA WANAWAKE KUWANIA NAFASI ZA UONGOZI

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog,
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa  Dar es Salam, umempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa utendaji kazi wake uliotukuka na kusema utendaji huo umeamsha zaidi ari ya Wanawake kuwania nafasi za uongozi kwa kuwa amethibitisha kwamba wanaweza tena kwa umahiri mkubwa.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa UWT  wa Mkoa huo Florance Masunga, wakati wa mkutano maalum wa Jumuiya hiyo kutoa tamko la kupongeza Rais Samia kutokana na Utendaji wake na namna alivyo dumisha amani, demokrasia Kitaifa na Kimataifa pamoja na kusimamia kikamilifu  tija kwa wafanyakazi.

“Alipokuwa akichukua  wadhifa wa kuwa Rais kulikuwa na manenomaneno. Lakini kwa utendaji huu anaouonyesha Rais Samia umetupa heshima wanawake, sasa sisi kazi yetu ni kumuunga mkono kwa kuyasema yale anayoyafanya, kwa dhati kabisa UWT Mkoa wa Dar es Salaam tunampongeza na tuko pamoja naye kwa kila hatua,” akasema Mwenyekiti Florence Masunga katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Ilala.

Alisema pia UWT  Dar es Salaam, imekoshwa na  hatua ya Rais Samia kudumisha amani, kusimamia vema Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa Mwenyekiti, kutangaza fursa za uwekezaji Kimataifa kupitia Filamu ya Tanzania The Royal Tour, kutoa nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi wa sekta ya umma, ujenzi wa miundombinu ya shule, ya Barabara, Madaraja na kutwaa tuzo ya kimataifa hivi karibuni mjini Accra Nchini Ghana.

Mwenyekiti Florence Masunga akasema pia UWT mkoa huo wa Dar es Salaam inampongeza Rais Samia kwa kugawa Sh. milioni 10 kwa Machinga kila mkoa, kusimamia kikamilifu  mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kwa Vijana, Wanawake na watu wenye ulemavu.

Aliwataka wanawake kusherehekea  mafanikio hayo ya Rais Samia kwa kugombea  nafasi za uongozi na kuchagua viongozi imara katika uchaguzi wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi na Jumiya zake unaoendelea.

Awali Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Angelina Akilimali, alisema uongozi wa Rais Samia  umeling’asrisha Taifa vya kutosha baada ya kutajwa katika jarida la Time kuwa miongoni mwa viongozi 100 wenye mvuto zaidi duniani kwa utendaji.

“Tunampongeza Rais Samia kwa ushindi wa tuzo na kutambulika Kimataifa kwa utendaji wake, kikubwa ninawaomba Wanawake wenzangu kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa CCM unaoendelea, msiogope, tumuunge mkono  Mwenyekiti wetu Rais Samia kwa kuchagua viongozi bora,”akasema Angelina maarufu kama Angel.

Naye Katibu wa UWT wa Mkoa huo wa Dar es Salaam Pauline Bupamba, akizungumza katika mkutano huo, amesema mafanikio yaliyopatikana katika uongozi wa Rais Samia ni yenye kutia moyo kwa kuwa mafanikio yanaonekana wazi hivyo amethibitisha kuwa wanawake wanaweza.

Paulina pia amesisitiza Viongozi wa CCM katika mkoa wa Dar es Salaam, kusimamia vema na kuhakikisha haki inatendeka katika uchaguzi unaoendelea wa kuwapata viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali, kwa kuwa ni jukumu la viongozi wanaosimamia uchaguzi huo kuhakikisha wanapatikana kwa haki viongozi bora.

"Kuna mahali imeshangaza sana, mwanachama kachukua fomu ya kugombea nafasi ya uongozi, lakini unakuta jina lake limekatwa kwa 'figisu' za hovyo. Kwa mfano unakuta kwenye fomu yake hakuna namba ya kadi yake ya CCM, kumbe imeondolewa  na viongozi kwa hila tu. Hii yaikubaliki.

Lazima wasimamizi wa uchaguzi huu watambue kwamba moja ya zawadi kubwa tunazopaswa kumpatia Mwenyekiti wetu wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan, ni kumpatia viongozi bora katika uchaguzi huu, ili waweze kumsaidia vema kukijenga chama chetu", akasema Paulina.

Mwenuyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga akizungumza katika Mkutano Maalum wa kumpongeza Rais Samia Suluhu Hasaan kwa uchakazi wake uliotukuka, uliofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Ilala, Jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Katibu wa UWT mkoa huo Paulina Bupamba na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Angelina (Angel) Akilimali.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Angelina(Angel) Akilimali akizungumza katika mkutano huo.
👆Wajumbe wakiwasikiliza Florence Masunga na Angelina (Angel) Akilmali wakati wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano huo.👇
*********************************

*******************

© June 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages