.
MH Jabir Shekimweri ni mkuu wa wilaya ya Dodoma ambapo amekuwa akifanya makubwa kwa wananchi wa wilaya hii kwa kuwaletea maendeleo na kuwasadia kutatua migogoro ya ardhi na changamoto zao mbalimbali.
Wilaya ya Dodoma ni wilaya ambayo inatakribani kata 41 ambapo tangu itangazwe kuwa makao makuu ya nchi na serikali kuhamia Mkoani Dodoma kumekuwepo na Ongezeko kubwa la wananchi na wageni mbalimbali ambao wamekuwa wakihamia mkoani hapa ili kuchangamkia fursa za kimaendeleo zilizopo mkoni hapa na hasa jijini Dodoma.
MH Shekimweri ili kuweza kuendana na kasi ya makao makuu ya nchi na kutekeleza sera ya MH RAIS Samia Suluhu Hassan ameamua kuingia mtaani kwa kufanya Ziara kwa kata kwa kata huku lengo kuu ni kuwafikia wananchi kwa ukaribu na kusikiliza kero zao na changamoto zao ili kuweZa kuwasadia kama kiongozi *mkuu wa ulinzi na usalamanna namsimamia wa maendeleo yote ya wilaya hii.Akiwa huko amekuwa akifanya mambo kadhaa
1. kufatiliamiradi yote ya maendeleo ambayo serikali imekuwa ikijenga kwenye wilaya hii na kuhakikisha miradi hiyo inatekezwa na kumalizika kwa wakati.
Ikumbukwe MH RAIS SAMIA SULUHU HASSAN aliweza kutoa zaidi ya Bilioni 300 ilikuweza kustawisha na kuuendeleza makao makuu ya nchi ikiwemo ujenzi wa Barabara ya mzunguko (Ring Road) ambapo katika mradi huu wa barabara utaambatana na uchimbwaji wa visima vikubwa vya maji katika kata nne za wilayani hapa,huku pia pakijengwa Vituo vya afya vitano jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaletea maendeleo wananchi wa Dodoma.
2.amekuwa akifanya vikao na wataalam wote wa kata(WDC) husika pamoja na wananchi huku akiwakumbusha umuhimu wa kuwajibika kila mmoja hasa kwa watendaji wa serikali ili kuwatatulia changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi huku pia akiwa elimisha wananchi hao kuchangamkia fursa za uwekezaji wilayani hapo ikiwemo kuwekeza kwenye biashara,Viwanda lakini kuilinda na kuithamini rasilimali ya ardhi ambayo kwa sasa inathamini kubwa kwa kuwaomba wajitahidi wazitunze na kuzitumia vizuri badala ya kuuza hivyo bila malengo na tija yoyote.
3. Amekuwa akitatua kero na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa tatizo kubwa kwa wananchi wilayani hapa ambapo kwa kiasi kikubwa ziara zake za kata kwa kata zimezaa matunda makubwa na kuweza kushirikiana na maafisa ardhi wa jiji la Dodoma kuweza kuwatatulia kero zao wananchi hasa hizi za ardhi ambapo ameweza kusaidia wananchi kupata haki zao ikiwemo hati za umiliki wa ardhi kwa wakati,kutatua migogoro iliyokuwepo ya malipo ya fidia kwa wananchi kwa maeneo ambayo yalitwaliwa na Serikali kwa ajili ya maendeleo.
Na katika kulipa uzito zaidi suala hili la migogoro ya ardhi amelitengea siku maalum ambapo kila siku ya Ijumaa ni siku maalumu ya kusikiliza na kutatua kero zote za migogoro ya ardhi ofisini kwake huku alishirikiana na maafisa ardhi wa jiji la Dodoma ili kuwaondolea adha na kadhia ya migogoro hiyo na kuhakikisha wanapata haki zao na stahiki zao.
4. Mh Shekimweri amekuwa akihamisha kwa kiasi kikubwa zoezi la utunzaji na uhifadhi wa Mazingira jijini hapa huku akishirikiana kwa karibu na idara ya mazingira ya jiji la Dodoma pamoja na wadau wote wa mazingira amekuwa ni muumini wa sekta hii kwani yeye mwenyewe ni mdau mkubwa wa mazingira kwa kiasi kikubwa jambo ambalo amekuwa akisimamia kwa weledi huku pia akitekeleza sera ya mazingira ya mwaka 2021 ambayo ilizinduliwa na MH Makamu wa Raisi Dkt Philip Mpango kwa kuwataka viongozi wote wa serikali na wananchi wote kutunza na kuhifadhi mazingira kwenye maeneo yao husika kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa.
5.amekuwa akinadi na kuutangaza utalii uliopo wilayani hapa hasa kupitia miradi ya kimaendeleo ambayo inajengwa kama vile Mji wa Magufuli(Magufuli City) uliopo Mtumba, Ujenzi wa Reli ya kisasa (Standard Geurge),Stendi kubwa ya kisasa ya Mabasi ya mkoani iliyopo Nzuguni 88,Ujenzi wa soko kubwa la Machinga (Machinga Complex),pia upatikanaji wa Zao maarufu la zabibu ambalo lipo mjini Dodoma na kumekuwa na mashamba makubwa ya zao hili maeneo ya mpunguzi,veyula,makutupora,n.k,zaidi akitangaza eneo maarufu la historia ya Mkoa wa Dodoma ambapo limetoa jina la mkoa huu la Dodoma kutokana na Tembo Kuzama eneo la Kikuyu na wenyeji kuita Idodomyia (Inayozama) eneo hili lipo Kikuyu ambapo ni eneo linaenda kuboreshwa na kutunzwa ili kuweka urithi na utalii wa ndani.
Kutokana na mambo haya Wanadodoma walishindwa kuficha hisia zao na kumuombea kwa Mungu huku wakimshuru kwa namna ambavyo anapigania na kutatua kero zao.
# DODOMA YA UTALII WA MIRADI
# DODOMA YETU ,MAENDELEO YETU
# DODOMA YA KIJANI INAWEZEKANA
# KARIBU UWEKEZE DODOMA
Malick Masoud
0683171771
Dodoma
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇