Jimbo la Musoma Vijijini lina Sekondari 22 za Kata/Serikali na 2 za Binafsi.
Upungufu wa Walimu ni mkubwa sana. Serikali inajitahidi kutoa ajira mpya na bado upungufu ni mkubwa.
WALIMU WA KUJITOLEA
Vijana wetu wanaosoma UDOM wako tayari kujitolea kufundisha kuanzia mwezi ujao, Julai 2022.
OMBI hilo limefikishwa kwa Mbunge wa Jimbo.
OMBI LA UPATIKANAJI WA POSHO ZA WALIMU WA KUJITOLEA
WAZALIWA au wenye chimbuko la Jimboni mwetu wanaombwa WAJITOKEZE kuchangia POSHO za hao vijana wetu waliotayari kufundisha kwa kujitolea.
Kiwango cha posho hizo, kwa ujumla wake ni kati ya Tshs 200,000 na 400,000 kwa mwezi. Makubaliano yatafanywa kati ya Uongozi wa Sekondari husika na Mwanafunzi anayejitolea.
Tunaomba walioko tayari kuchangia posho hizo wajitokeze.
Mchangiaji anaweza kuchagua Sekondari anayopenda kuchangia na Ofisi ya Mbunge itamuunganisha na chaguo lake.
Orodha ya WACHANGIAJI ikipatikana VIONGOZI wa Wanafunzi hao (UDOM) watapewa taarifa.
Waliokuwa tayari kuchangia wawasiliane moja kwa moja na Mbunge wa Jimbo
Namba:
+255 754 400 800
Wengine wanaweza kuwasiliana moja kwa moja na Sekondari wanazopenda kuzichangia.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumamosi, 11.6.2022
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇