Mtwara, Juni 5, 2022
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mtwara kutomfumbia macho mfanyabiashara wa pembejeo anayetumia vibaya jina la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuuza pembejeo 'feki' za kilimo.
Shaka ametoa ombi hilo wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara, ambapo amesema mfanyabiashara huyo (ambaye hakumtaja) amekuwa akiuza pembejeo zisizokidhi viwango (Feki) huku akidai ni mali ya Waziri Mkuu Majaliwa jambo ambalo sio kweli.
Amesema kwa kufanya hivyo mfanyabiashara huyo anafanya hujuma dhidi ya juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kuwasaidia wakulima ambapo serikali inagawa bure pembejeo hizo.
"Na isivyo bahati sana mfanyabiashara huyo anatumia jina la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwamba eti hiyo ni mali ya Waziri Mkuu na yeye amepewa uwakala na Waziri Mkuu. Vyombo vya ulinzi na usalama huyo mtu bado yupo tu mtaani kweli!.
Kweli huyo mtu bado yupo tu mtaani, sijui kwa sababu ana nguvu ya fedha, sijui kwa kweli, na bahati nzuri nilipopata taarifa na nikapata ushahidi nilimtafuta Waziri Mkuu, nikamwambia Mheshimiwa Waziri Mkuu, akaniambia katika hili huyo mtu aje athibitishe, akasema Shaka.
"Sijawahi kufanya biashara ya pembejeo si Mtwara, sio sehemu yoyote sihusiki na hilo jambo na mie nashangaa vyombo vya Ulinzi na usalama havijamtia mkononi bado, na anasambaa ndani ya Mkoa huu wa Mtwara," akasema Shaka akikariri jibu la Waziri Mkuu Majaliwa.
Kwa mujibu wa Shaka ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, miongoni mwa wahusika wa 'mchezo' huo mchafu wa biashara ya pembejeo feki, wamo baadhi ya madiwani ambapo ameisitiza kuwa Chama hakitamvumilia kiongozi yeyote atakayethibitika kufanya uhalifu.
Shaka amewataka viongozi wa CCM mkoani Mtwara kuhakikisha wanasimamia shughuli ya usambazaji wa pembejeo hizo na kutekeleza dhamira njema ya Rais Samia kwa wananchi.
Your Ad Spot
Jun 6, 2022
Home
featured
siasa
SHAKA AVITAKA VYOMBO KUMSHUGHULIKIA ANAYEUZA PEMBEJEO FEKI, AKIONGOPA KUWA NI MALI YA WAZIRI MKUU
SHAKA AVITAKA VYOMBO KUMSHUGHULIKIA ANAYEUZA PEMBEJEO FEKI, AKIONGOPA KUWA NI MALI YA WAZIRI MKUU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇