LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 4, 2022

SHAKA AHIMIZA WATANZANIA KUWEKA AKIBA YA CHAKULA ILI KUWA TAYARI KUKABILIANA NA TISHIO LA NJAA LINALOINYEMELEA AFRIKA

Nanyamba, Mtwara
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amewahimiza Watanzania kutumia vizuri chakula ili kukabiliana na tishio la njaa linalolinyemelea Bara la Afrika.

Shaka ametoa mwito huo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi katika maeneo mbali mbali  Wilayani Tandahimba na Halmashauri ya Nanyamba  mkoani Mtwara akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezani wa Ilani ya CCM na uhai wa Chama.

“Ndugu zangu shirika la chakula duniani limetangaza tahadhari ya hali ya chakula duniani. Kwahiyo naomba tuweke akiba ya chakula” alisema Shaka na kuongeza

“Nchi kadhaa zimetangaza hali ya hatari  hao wanaoshughulika na chakula duniani(Wfp) wanasema watu zaidi ya milioni 80 Afrika wako kwenye hatari hiyo”

Amesema vita vya Ukraine vimechangia hali hiyo.” Mnasikia kwenye vyombo vya habari vita huko Ukraine vimesababisha upungufu wa ngano kwasababu asilimia takriban 40 ngano inatoka huko”.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na wananchi mkoani Mtwara, leo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages