LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 28, 2022

SAFARI ZA TRENI YA SGR DAR ES SALAAM - MOROGORO KUANZA SEPTEMBA MWAKA HUU

Na CCM Blog, Dodoma

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete amesema safari za reli ya kisasa ya Standard Gauge (SGR) ya kilometa 300 kati ya Dar es Salaam na Morogoro zitaanza rasmi mwezi septemba mwaka huu.


Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Dk. Christine Ishengoma aliyetaka kujua ni lini safari zitaanza, Naibu Waziri amelieleza Bunge kuwa kwa sasa kinachoendelea ni majaribio ya mifumo ya umeme na vituo.


Naibu Waziri Mwakibete amesema katika hatua ya kuelekea kufanikisha hilo, mabehewa na vichwa vya treni hiyo ya kisasa vinatarajiwa kuwasili nchini mwezi Agosti 2020.


Amesema Serikali ya awamu wa sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha Sh. trilioni 6.5 kwa wakandarasi wote wanaojenga reli hiyo na kutoa kandarasi zenye thamani ya Sh. trilioni 15 na kumpongezs Rais Samia kwa hatua hiyo.


“Reli ya Dar es Salaam hadi Morogoro (Km 300) itaanza rasmi mwezi wa tisa na kwamba mwezi wa nane yataingia mabehewa na vichwa. Kinachofanyika sasa hivi ni majaribio ya umeme, vituo na signals,” amesema Naibu Waziri.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages