RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema
Mkoa wa Kagera una fursa kubwa ya kiuchumi na kibiashara, hivyo unapaswa
kupewa kipaumbele katika mipango na mikakati ya maendeleo.
Rais
Samia amesema hayo wakati akizungumza na Wananchi katika mkutano wa
hadhara uliofanyika katika uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.
Aidha,
Rais Samia amesema, Mkoa wa Kagera ni wa kimkakati katika kuinua uchumi
wa nchi kwa kuwa unapakana na nchi za Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya.
Kwa
upande mwingine, Rais Samia ametoa onyo kwa Vyama vya Ushirika kuacha
kunyonya wakulima wa kahawa mkoani humo na kuwaacha wauze mazao yao
kulingana na bei wanayoitaka.
Rais Samia pia, amesema bei ya mauzo ya kahawa haipaswi kuwa na makato kwa kuwa Serikali inatoa ruzuku katika pembejeo.
Halikadhalika,
Rais Samia amewataka Waziri wa Ardhi pamoja na Waziri wa Mifugo na
Uvuvi kushughulikia changamoto ya uhaba wa malisho na uwepo wa migogoro
ya ardhi katika baadhi ya maeneo mkoani humo.
Kuhusu
uvuvi, Rais Samia amesema Serikali inafanya jitihada ya kuinua sekta ya
hiyo ikiwemo kununua boti na kuongeza fedha kwenye mfuko wa uvuvi kwa
wavuvi wadogo ili kuwakomboa kuwainua kiuchumi.
ZuhuraYunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇