Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo ameenda kumjuilia hali Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam.
Dkt. Kikwete amempongeza Mzee Mwinyi kwa kutimiza umri wa miaka 97 na amefurahi kumkuta mwenye afya njema na uso wa tabasamu. Amemuombea umri mrefu wenye afya tele, furaha, baraka na fanaka.
Ni nchi chache duniani kuona jambo kama hili la viongozi wastaafu wakiishi kwa amani na upendo. Tanzania tumejaaliwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇