LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 23, 2022

PROF. NDAKIDEMI AOMBA SERIKALI IWAPELEKEE WAKULIMA WA KAHAWA MAJI, MICHE NA PEMBEJEO

 Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi ameishauri serikali kuwapelekea wakulima wa zao la kahawa maji kwa ajili ya umwagiliaji, miche bora na pembejeo ili uzalishaji uongezeke.


Aidha, Prof Ndakidemi ameipongeza serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa miradi lukuki katika jimbo lake la Moshi Vijijini.

Prof. Ndakidemi ametoa ushauri huo alipokuwa akitoa mchango wake katika mjadala wa hali ya uchumi wa Taifa na mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali bungeni Dodoma Juni 22, 2022.


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, akitoa pongezi na ushauri wake huo....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages