Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ametoa ushauri ufuatao wakati alipokuwa akichangia Mpango & Bajeti ya Mwaka 2022/2023.
Ameshauri:
*Uchumi ukue kwa kiwango cha 8-10% ili kupunguza umaskini kwa kasi kubwa.
Sekta zinazoweza kukuza uchumi kwa kiwango hicho na zinahitaji uwekezaji mkubwa ni:
*Kilimo, Uvuvi & Ufugaji (ichangie: 1-2% growth)
*Utalii (ichangie: 1% growth)
*Madini + Helium (vichangie: 3-4% growth)
*Uchumi wa Gesi Asilia + uuzaji wa umeme nje (vichangie: 5-6% growth). Tuna Gesi Asilia kiasi cha 57.54 tcf
Mbunge huyo ameeleza maana ya Uchumi Gesi Asilia (Natural Gas Economy) na kuendelea kushauri TPDC ifanye kazi yake muhimu ya kutafuta GESI & MAFUTA nchi mwetu, k.m. kule Ruvuma Basin Msumbiji imegundua 100 tfc za Gesi Asilia na huenda inayo 200 tfc. Je upande wa Tanzania ipo kiasi gani?
Je Ziwa Tanganyika ipo gesi au mafuta? Ziwa Nyasa je? Ziwa Rukwa? Ziwa Eyasi? Bahari Kuu (Indian Ocean) kuna gesi kiasi gani? Mafuta?
Tafadhali msikilize Prof Sospeter Muhongo kwenye CLIP/VIDEO kutoka Bungeni. Imeambatanishwa hapa.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Alhamisi, 16.6.2022
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇