Na Dismas Lyassa
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ndg. Ridhiwani Kikwete amemkabidhi Mh. Waziri wa Utalii Ndg. Pindi Chana kwa niaba ya Wananchi wa kaya 23 zenye watu wapatao 113, Hati ya Makazi na Mashamba 23 , Vitalu 6 vya Malisho vyenye ukubwa wa Hekta Elfu 22, maeneo ya Viwanja na mashamba yaliyopimwa 5230 yaliyokwishapima 14579.
Alifanya hivyo wakati wa hafla ya kuwakaribisha Wananchi wapya wa Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga Tarehe 16 Juni 2022 katika kijiji cha Msomera mpakani Mwa Wilaya ya Handeni na Kilindi, Mkoa Tanga.
Wananchi walifurahishwa na tukio hilo huku baadhi yao wakishangilia kumpongeza Mh.Kikwete kwa kufuatilia kero za ardhi na kuzichukulia hatua haraka.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ndg. Ridhiwani Kikwete (wa pili kutoka kulia mwenye kofia na saa) akiwa kwenye tukio la kukabidhi hati ya ardhi.
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye tukio la Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ndg. Ridhiwani Kikwete kukabidhi hati ya ardhi
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇