LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 24, 2022

MHARIRI NA MTUMISHI MWANDAZI MSTAAFU WA CCM GABRIEL ATHUMAN AMEFARIKI DUNIA

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog

Mwandishi wa habari ngazi ya Mhariri  na Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Itikadi na Uenezi mstaafu Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Gabriel Athuman, amefariki dunia.

 

Habari zimesema, Gabriel aliyezaliwa Septemba 25, 1960, amefariki mjini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.

 

Gabriel katika kazi ya Uandishi wa Habari amewahi kuwa Mhariri wa Habari kabla ya kuhamia Makao Makuu ya CCM kuwa Afisa Habari katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM zaidi ya miaka 20 iliyopita.

 

Wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 Gabriel alikuwa ndiye Mratibu Mkuu wa Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari, waliokuwa wakiandika habari katika Misafara ya Kampeni za CCM upande wa Mgombea Mwenza ambaye wakati huo alikuwa ni Rais wa sasa Samia Suluhu Hassan. Msaidizi wa Gabriel alikuwa ni Bashir Nkoromo.


Msimamizi Mkuu wa Blog ya Taifa ya CCM kwa niaba ya timu nzima, anatoa pole za dhati kwa waliokuwa safanyakazi wenzake CCM, Waandishi wa Habari, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu.

 

Sote ni wa Mungu, kwake sote tutarejea.

Gabriel Athumani enzi za uhai wake.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages