LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 26, 2022

MAKAMU WA RAIS DK. MPANGO AWASILI JIJINI LSBON, URENO, LEO

Lisbon, Ureno

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango amewasili  leo mjini Lisbon nchini Ureno kumwakilisha Rais  Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Pili wa Umoja wa Mataifa kuhusu Uhifadhi wa Bahari na Rasilimali zake.


Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Makamu wa Rais imesema, lengo la Mkutano huo ni kuhamasisha juhudi za Mataifa katika kufanikisha utekelezaji wa Lengo la 14 la Maendeleo Endelevu na Mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya Tabianchi.

 

Mkutano huo unatarajiwa kuanza kufanyika kesho Juni 27, hadi  Julai Mosi 2022 Jijini Lisbon na kuhudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa, Wadau wa Mazingira pamoja na Wakuu wa Taasisi mbalimbali duniani.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages