Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa, amesema kuwa Tanzania inatarajiwa kuwa na ziada ya umeme hivyo kinachotakiwa ni kujikita katika usafirishaji na usambazaji wa umeme vijijini. Aidha, Kawawa amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa sh. bil. 100 ikiwa ni ruzuku iliyosaidia kupunguza bei ya mafuta nchini na kwamba hivi sasa bei ya mafuta nchini inaweza kuwa ya chini kuliko nchi zote za Afrika Mashariki na Kati. Ametoa ushauri na pongezi hizo alipokuwa akichangia mjadala wa makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Nishati bungeni Dodoma Juni Mosi, 2022.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Kawawa akitoa pongezi na ushauri wake huo....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇