Stockhilm, Sweden
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango amewataka Watumishi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden kuongeza maeneo ya ushirikiano baina ya Tanzania na nchi hiyo ili kuchangia vema katika diplomasia ya uchumi.
Makamu wa Rais amesema hayo leo Juni 4, 2022 alipotembelkea Ubalozi wa Tanzania nchini humo uliopo Mjini Stockholm na kuongeza kwamba ni vema kudumuisha mahusiano mazuri yaliopo baina ya mataifa hayo mawili ambao umedumu kwa muda mrefu.
Amesema nchi ya Sweden imekua rafiki kwa Tanzania katika nyanja mbalimbali kama vile katika sekta ya Elimu, Utawala bora pamoja na Uchumi. Aidha amewasihi kutafuta zaidi ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji pamoja na fursa za za masomo zitakazosaidia katika kuwajengea uwezo watanzania wa kufanya kazi.
Makamu wa Rais ameuagiza Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden kuhakikisha wanajenga mtangamano kwa watanzania wanaoishi Sweden pamoja na maeneo mengine ya uwakilishi ili waweze kuwa na mchango katika ujenzi wa Tanzania.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mheshimiwa Grace Olotu amesema Ubalozi huo utaendelea kuwatumikia watanzania katika maeneo yote ya uwakilishi kwa kuitangaza na kuhakikisha wanaendeleza diplomasia ya uchumi kwa tija kubwa kwa manufaa ya taifa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango, akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Balozi wa Tanzania nchini Sweden, alipotembelea Ubalozi huo leo Juni 4, 2022.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇