LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 23, 2022

DIRISHA LA USAJILI KWA KLABU ZA LIGI KUU YA NBC CHAMPIOSHIP, FIRST LEAGUE KUFUNGULIWA JULAI 1, 2022

 
   Dirisha la usajili kwa Klabu za Ligi Kuu ya NBC, Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite msimu wa 2022/2023 litafunguliwa Julai 1, 2022 na kufungwa Agosti 31, 2022.

Katika kipindi hicho Klabu zinatakiwa kukamilisha usajili na uhamisho wa Kimataifa.

Klabu zote zinapaswa kuzingatia muda huo wa usajili, hakutakuwa na muda wa ziada baada ya dirisha kufungwa. Yeyote atakayekutana a changamoto awasiliane na Idara ya Mashindano TFF.

Aidha Dirisha Dogo lenyewe litafunguliwa Desemba 16, 2022 na kufungwa Januari 15, 2023.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages