LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 5, 2022

BALOZI DKT CHANA: SOMENI KWA MAKINI TAKWIMU ZA USIMAMIZI SHIRIKISHI WA MISITU







Wadau wa misitu nchini wametakiwa kusoma kwa makini  takwimu za usimamizi shirikishi wa misitu ili kupata picha ya hali halisi iliyopo  sasa kuhakikisha kuwa wanatekeleza Mpango Kazi wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu.


 Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana Jijini Dodoma wakati akizindua  Mpango Kazi wa Kitaifa wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu na Takwimu za usimamizi shirikishi wa Misitu ya Jamii.


Dkt. Chana alisema kuwa Tanzania inapoteza takribani hekta 469,000 za misitu kila mwaka akiongeza kuwa kama juhudi za pamoja hazitachukuliwa kuna hatari ya nchi  kuanza kupata athari za kimazingira  ambazo huathiri nchi yetu na dunia kwa ujumla.


Aidha, amewahimiza wamiliki wa misitu ya Jamii ikiwemo ya vijiji kuisimamia kikamilifu kulingana na Sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo akisisitiza kuwa iwapo mpangokazi aliouzindua  utatekelezwa ipasavyo, utawezesha uhifadhi na matumizi endelevu misitu ya jamii na pia kuchangia maendeleo endelevu katika sekta nyingine.


”Ili nyaraka hizi zieleweke vyema na  kutumika kwa ukamilifu miongoni mwa wadau walio wengi, ninaiagiza Idara ya Misitu na Nyuki izifanyie tafsiri nyaraka hizi  ziwe kwa lugha ya kiswahili na zisambazwe kwa wadau wengi kwa kadri itakavyowezekana”.Aliongeza Balozi Dkt Chana

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages