LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 22, 2022

WIZARA YA ELIMU YAWATAKA VIJANA KUWA MABOLOZI WAZURI VIJIJINI KUELEZA UMUHIMU WA SENSA+video

 Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Hosea Kennedy amewaalika wanafunzi wanachama wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo na Vyuo Vikuu (TAHLISO) kushiriki katika makongamano ya kutoa maoni kuhusu mabadiliko ya sera na mitaala ya elimu.

Aidha amewataka vijana hao kushiriki vyema kutoa elimu juu ya umuhimu wa sensa katika maeneo yao. Kennedy ameyasema hayo wakati wa Kongamano lililoandaliwa na TAHLISO kuhusu umuhimu wa Sensa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma Mei 21, 2022. Kongamano hilo lilihudhuriwa pia na Kamisaa wa Sensa, Spika mstaafu, Anne Makinda.

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Kennedy akizungumza katika mkutano huo....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages