Msaidizi Mkuu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mwakalukwa Leonard amewataka vijana nchini kutumia mitandao ya kijamii kuelimisha na kufikisha elimu ya sensa kwa wananchi. Aidha amesema kuwa kwa upande wa idara yao kwa kushirikiana pia Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) hadi sasa wameshafanya makongamano 30 ya kuhatoa elimu na kuhamasisha wananchi kushiriki sensa Agosti 23, mwaka huu. Ameyasema hayo wakati wa Kongamano la TAHLISO Mkoa wa Dodoma la Umuhimu wa Sensa lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete na kuhudhuriwa na Kamisaa wa Sensa, Spika mstaafu Anne Makinda Mei 21, 2022.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mwakalukwa pamoja na na mambo mengine akihamasisha vijana kushiriki kutoa elimu ya umuhimu wa sensa.....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇