Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama (kushoto) akimkabidhi hatimiliki ya ardhi ya kimila mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Makanda na Msisi katika hafla ya kukabidhi hati na kuweka mawe ya msingi ya ujenzi wa majengo ya ofisi za masijala katika vijiji hivyo wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma Aprili 30, 2022.
Waziri Mhagama akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Dkt Seraphia Mgembe baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la ofisi za masijala katika Kijiji cha Msisi ambapo MKURABITA ilikipatia kijiji hicho zaidi ya sh. mil. 40 kumalizia ujenzi huo.
Waziri Mhagama akiweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la ofisi za masijala katika kijiji cha Makanda wilayani Bahi. MKURABITA imekipatia kijiji hicho zaidi ya sh. mil. 36 kumalizia ujenzi huo.
Mkurugenzi wa Urasimishaji Ardhi na Biashara wa MKURABITA, Jane Lyimo akitoa utambulisho watendaji wa mpango huo.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda akitoa shukrani kwa MKURABITA kufanikisha urasimishaji ardhi katika vijiji hivyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa MKURABITA, Dkt Seraphia Mgembe akielezea kuhusu kazi ya urasimishaji ilifanyika kwa muda mfupi katika vijiji hivyo kwa kuwashirikisha ipasavyo wananchi kutekeleza majukumu.
Waziri Mhagama akihutubia wakati wa hafla hiyo katika Kijiji cha Msisi.
Wananchi wakionesha furaha kwa kushangilia wakati Waziri Mhagama akihutubia.
Waziri Mhagama akiondoka baada ya kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa jengo la masijala katika Kijiji cha Msisi.
Waziri Mhagama akipokea risala kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Makanda,
Mbunge wa Bahi, Kenneth Nollo akihutubia wakati wa hafla kwa kuishukuru MKURABITA kufanikisha urasimishaji ardhi katika vijiji hivyo..
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, ujue yaliyojiri katika hafla hiyo...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDAMHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇