Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi akitoa maoni yake katika mkutano wa wabunge kutoa maoni kuhusu maboresho ya sera na mitaala nchini, ameshauri kuwa tusiache kabisa lugha ya kiingereza kufundishia, ama sivyo tutapigwa goli katika medani ya kimataifa.
Aidha, akiendelea kutoa maoni hayo katika mkutano ulioandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika Ukumbi wa Msekwa, Bungeni Dodoma Mei 7, 2022, ameshauri kuwa katika maboresho hayo yaongozwe masomo ya ujasiriamali na ubunifu ili kumuandaa mwanafunzi kujiajiri.Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Prof. Ndakidemi akitoa maoni yake hayo....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇