LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 22, 2022

NCCR-MAGEUZI YAMSIMAMIZSHA KAZI MWENYEKITI WAKE MBATIA, KISA UKIUKWAJI WA MAADILI

Na CCM Blog, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara Angelina Mtaigwa leo Mei 21, 2022 wamesimamishwa uongozi na Halmashauti Kuu ya Chama hicho kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ukiukwaji wa maadili.

Akisoma maazimio ya Halmashauri Kuu ya NCCR- Mageuzi katika Mkutano kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam, leo Mwenyekiti wa hikao hicho Joseph Selasini ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, amedai Mbatia amesimamishwa Uenyekiti kutokana na kutokuwa na mahusiano mazuri na makatibu wake.

“Tulielezwa jinsi ambavyo Mwenyekiti alimtaka Katibu Mkuu ajiuzulu na ikumbukwe hana zaidi ya mwaka ndani ya chama na katika mjadala tumekubaliana alikuwa anabadilisha Makatibu Wakuu jinsi anavyotaka. Sasa huyu ni Katibu wa sita tangu alivyokuwa Mwenyekiti,” amedai Selasini.

Selasini ametaja sababu nyingine za Mbatia kusimamishwa kuwa anatuhumiwa kukisabisha chama hicho kisishiriki mikutano mbalimbali iliyotitishwa kwa ajili ya kujadili masuala ya demokrasia ya vyama vingi, ikiwemo ulioitishwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).

Amedai, awali chama hicho kilikataa kushiriki vikao hivyo hadi Serikali itakapokuwa na nia njema dhidi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani, ikiwemo kuachwa huru kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, aliyekuwa rumande katika Gereza la Ukonga, kwa tuhuma za ugaidi.

Selasini amedai, baada ya Mbowe kuachwa huru Machi 2022, NCCR-Mageuzi haikuwa na kikwazo cha kushiriki vikao hivyo lakini Mbatia aliitisha kikao cha kamati cha dharura kubatilisha uamuzi huo.

Selasini amedai maazimio ya halmashauri hiyo kumsimamisha Mbatia ni halali, kwani akidi ya wajumbe wake ilikidhi matakwa ya kisheria ambapo waliohudhuria ni 52 kati ya wajumbe 82.

“Kabla ya mjadala haujaanza ulizuka mjadala wa Mwenyekiti wa chama kutokuwepo katika mkutano huu na taarifa ilitolewa kwamba anazo taarifa za mkutano akishiriki kuuitisha na baada ya kusubiri kwa muda bila kujulikana na wajumbe wako tayari ukumbi tukaona mkutano uendelee,” amesema Selasini.

Akizungumzia uamuzi huo, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, amesema utaratibu uliotumika kuchukua hatua hiyo ni halali kwa kuwa ulifuata sheria.

“Kimsingi nilikuwepo, nimeona akidi imesomwa wajumbe wapo na walijitamulisha na sisi tuna orodha yetu ya wajumbe ofisini, kwa hiyo tutaenda kulinganisha na tulio nao ofisini,” amesema Nyahoza na kuongeza:

“Kwa jinsi akidi ya wajumbe ilivyosomwa imetimia na kama imetimia kikao ni halali na utaratibu umefuatwa kwa mujibu wa sheria wa kuwasimamisha.”

James Mbatia

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages