LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 21, 2022

HALIMA KOPWE MISS TANZANIA , RAIS SAMIA KUJENGA UKUMBI WA KIMATAIFA JIJINI DAR

 







 
Na John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Serikali ya Mhe. Rais Samia imedhamiria kuinua kuinua kiwango cha mashindano ya urembo nchini  ikiwa ni pamoja na kujenga ukumbi wa
kimataifa  katika jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza usiku wa kuamkia leo Mei 21, 2022 kwenye kilele cha mashindano ya
kumtafuta  Miss Tanzania 2022 ambapo Halima Kopwe toka Mtwara ametwaa
taji hilo, Mhe . Mchengerwa amesema ukumbi huo  licha ya kufanyiwa kazi
mbalimbali za Sanaa na burudani pia utatumika kwenye mashindano ya  kimataifa
 ikiwa ni pamoja na shindano la Miss Tanzania.

 “Ukumbi huo unatarajiwa kuongoza kwa ubora na ukubwa barani Afrika ambapo
utachukua takribani watu elfu ishirini” amesisitiza Mhe. Mchengerwa
Aidha,
amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuwashika mkono washindi
wote na kufafanua kuwa washiriki wote walioshiriki shindano hili hadi
kufika fainali ni washindi.
Amewapongeza
waandaji wa shindano hilo kwa uratibu mzuri  ambapo ameongeza kuwa
washiriki  wamefanya kazi nzuri ya ubunifu na Sanaa.
Pia amesema Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ndiyo Wizara pekee inayowapa furaha na faraja watanzania wengi.

Pia Mhe. Mchengerwa amesema Filamu ya Royal Tour imesaidia kufungua milango na kuitangaza Tanzania  duniani na kuwataka wasanii kutumia fursa hiyo
kutengeneza ajira na vipato.

Miss Tanzania kwa mwaka huu; Halima Kopwe amejishindia gari  dogo aina ya
Benzi lenye thamani ya shilingi milioni 30 na  fedha taslimu shilingi milioni kumi.

Shindano hilo limefanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Mlimani City na kuhudhuriwa na mamia ya washabiki wa urembo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages