LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 18, 2022

MWENYEKITI WA CCM, RAIS SAMIA ATEMBELEA OFISI YA CCM MKOA WA TABORA LEO, AZUNGUMZA NA KAMATI YA SIASA YA MKOA HUO

Tabora, leo
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Kamati ya Siasa ya CCM mkoa wa Tabora alipotembelea Ofisi ya CCM ya mkoa huo, leo.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Shaka Hamdu Shaka imesema, pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa CCM Rais Samia alipokea taarifa ya mwenendo wa uchaguzi wa ndani ya chama unaoendelea na kujadiliana masuala mbalimbali yenye ustawi na CCM na wananchi wa Tabora kwa ujumla.

"Awali Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Ndg Hassan Wakasuvi akimkaribisha  Mwenyekiti, Rais alimueleza kuwa Chama Cha Mapinduzi mkoani Tabora na wananchi kwa ujumla wanaridhishwa na utendaji wa serikali anayoiongoza katika kuimarisha utoaji huduma, ujenzi wa miundombinu na ukuzaji wa uchumi kwa wananchi mkoani humo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025", imesema Taarifa hiyo.

"Nimekuwa mwanachama wa chama hiki na kiongozi kwa miaka 25 lakini tukio la Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea ofisi za chama chetu na kuzungumza na viongozi wake hili ni tukio la kwanza kwa mkoa wa Tabora. Haya ni mahusiano mazuri baina ya chama na serikali, tunakushukuru sana na tunakukaribisha Tabora." Taarifa imemkunuu Wakasubi akisema.

Rais Samia Suluhu Hassan yupo mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku tatu aliyoianza tarehe 17 Mei, 2022 na ataihitimisha tarehe 19 Mei, 2022 kwa kuwahutubia wananchi wa mkoa wa Tabora katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Samia Suluhu Hassan , akipokewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora (Mwenye kofia) Hassan Wakasuvi, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi  Shaka Hamdu Shaka na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dk. Batilda Buriani alipowasili Ofisi Za CCM Mkoa wa Tabora, leo asubuhi, Mei 18 , 2022.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Samia Suluhu Hassan, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Ofisi ya CCM mkoa wa Tabora leo asubuhi Mei 18 , 2022.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Tabora alipotembelea Ofisi ya CCM mkoa huo leo asubuhi Mei 18 , 2022.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Tabora wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizungumza nao leo asubuhi Mei 18, 2022. Kula (walioketi mbele ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Chaka Hamdu Shaka.


 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages